Muamala kwa Shule za Qur'an: Kwa Mara Nyengine Tena ni Dhihirisho la Sera dhidi ya Uislamu
- Imepeperushwa katika Uholanzi
- Kuwa wa kwanza kutoa maoni!
- |
Serikali imekubali mpango ambao Waziri wa Elimu Dennis Wiersma anataka kuutekeleza kwa shule za Qur'an, shule za wikendi na maeneo mengine ambayo 'elimu isiyo rasmi' inatolewa. Ufafanuzi kutoka kwa Wizara wa mpango huu wa kibaguzi ambao kwao Waislamu wanatengwa ni kwamba ndani ya elimu isiyo rasmi kumekuwa na kesi zinazodaiwa za shughuli ambazo 'zinapinga na uoanishaji, zinapinga demokrasia dhidi ya utawala wa sheria.'