Jarida la Al-Waie: Vichwa Vikuu vya Habari vya Toleo (470)
- Imepeperushwa katika Jarida la Al-Waie
- Kuwa wa kwanza kutoa maoni!
Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir inafuraha kuwasilisha kwa wafuasi na wanaozuru kurasa za Afisi Kuu Habari DVD mpya katika lugha tatu yenye kichwa: “Nasheed za Khilafah 1447 H - 2025 M”
Milipuko ya mabomu inateketeza miili ya watoto mjini Gaza, njaa inatafuna mabaki yao, mizinga inasaga saga uhai na nyumba za watu walio na msimamo thabiti, na ndege zinanyesheza lava zao kwenye hospitali na hema za waliohamishwa. Kutokana na hali ya uhalifu huu, kongamano lililokongamana jana usiku, 22 Septemba 2025, jijini New York, lililoitishwa na Ufaransa na Saudi Arabia, lilitaka kutambuliwa kwa “Dola ya Palestina”.
Maradhi matatu ya kimazingira—kipindupindu, homa ya dengue, na malaria—yanawaangamiza watu katika majimbo ya Khartoum, Al-Jazirah, na Darfur, katikati ya uzembe wa kutisha na aibu ya kukosekana kwa serikali inayojiita “Serikali ya Matumaini”! Kuna matumaini aina gani wakati watu wanaishi katika mazingira yasiyostahili hata kwa wanyama—mazingira yanayotawaliwa na waenezaji magonjwa, ikiwemo mbu wa malaria, mbu wa dengue, na nzi?
Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir katika Wilayah Sudan inafuraha kuwaalika wanahabari, wanasiasa, na wale wote wanaopenda masuala ya umma, kuhudhuria na kushiriki katika kikao kipya cha Kisiasa, ambapo Ustadh Ya‘qub Ibrahim, mwanachama wa Hizb ut Tahrir/Wilayah Sudan, atakuwa mgeni, chini ya kichwa: Ulaya na Ushawishi Wake kwa Matukio nchini Sudan.
Hizb ut Tahrir ni chama cha kisiasa ambacho mfumo wake ni Uislamu, kinataka kurudisha mfumo kamili wa maisha ya Kiislamu kwa kusimamisha Khilafah Rashida ya pili kwa njia ya Utume kwa njia ya kisiasa, na hakitekelezi vitendo vyovyote vya kisilaha si kwa kumwogopa mtu yeyote, bali ni kujifunga na njia ya Mtume (saw) katika kusimamisha dola ya kwanza ya Kiislamu.
Kwa mara nyingine tena utawala wa Marekani unaonyesha sura yake halisi kupitia taarifa za mjumbe wake Tom Barrack, katika mahojiano yake yaliyotangazwa na Sky News na mtangazaji mkuu wa IMI International Hadley Gamble, ambaye alijiruhusu kuingilia waziwazi katika masuala ya Lebanon na kubainisha sifa za dori za taasisi ya Jeshi.
Baada ya hotuba ya rais wa Marekani kwenye Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa – ambayo asili ilikusudiwa kuhakiki kadhia ya Palestina – na katika wakati ambapo, kwa msimamo mmoja kutoka zaidi ya dola 150 kati ya dola 193 za Umoja wa Mataifa, “dola ya Palestina” tayari imetambuliwa, Rais Trump aliikejeli jumuiya ya kimataifa kwa kuyaita maneno ya “viongozi” kama “domo tupu.” Pia alikejeli makubaliano ya kimazingira, akaiichukulia mikataba ya uhamiaji kuwa ya kudharauliwa, na akakashifu mchakato wa Ulaya wa kuitambua Palestina kwa kuiita udhaifu. Hotuba yake ilionekana kama dua ya mwisho ya mazishi (fatiha) iliyosomwa juu ya makubaliano ya kimataifa, madai ya mtazamo wa upande mmoja wa Amerika katika masuala ya kimataifa, na tangazo la kulazimisha rai yake juu ya Mashariki ya Kati – haswa suala la Palestina.
Uingereza, Canada, Australia na Ureno zililitambua ile inayoitwa “Dola ya Palestina,” na kufuatiwa na nchi kadhaa katika mkutano wa ngazi ya juu wa kimataifa wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa uliofanyika kuanzia Septemba 22-30, 2025, na ulioongozwa na Ufaransa na Saudi Arabia. Utambuzi huu ulikaribishwa na watawala Ruwaibidha (wajinga wasio na maana) wa Waislamu, pamoja na Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu na Jumuiya ya Waarabu. Jambo la kushangaza ni kwamba, ilikaribishwa pia na mashirika ya Kipalestina, ambayo yanaona kuwa ni matunda ya uthabiti wao, kana kwamba Palestina imekombolewa na na umbile la Kiyahudi kung'olewa!