Jumapili, 22 Muharram 1446 | 2024/07/28
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Barakoa Zimepomoka: Miaka 76 ya Ukaliaji Kimabavu wa Ardhi Iliyobarikiwa ya Palestina

Palestina haitakombolewa kwa kujifunza kuhusu historia yake. Kususia, kutengwa na vikwazo havitaikomboa Palestina. Palestina haitakombolewa kwa msaada wa chakula. Palestina itakombolewa wakati wana shupavu wa Umma katika majeshi ya Waislamu watakapowaasi watawala wasaliti, wakavunja minyororo yao na kuandamana kuelekea Al Quds.

Soma zaidi...

Serikali Kuchimba Migodi katika Eneo linaloishi Viumbe Hai (Biosphere) ni Dhulma kwa Umma!

Rais Sadyr Japarov alifanyia marekebisho sheria kuhusu “maliasili zilizo chini ya ardhi” na “maeneo yanayoishi viumbe hai (biosphere)” ambapo utafiti wa kijiolojia na utafiti katika maeneo ya yanayoishi viumbe hai (biosphere), uchunguzi wa kijiolojia wa rasilimali za dunia, uchimbaji wa akiba muhimu na kazi ya uchunguzi wa kijiolojia kwa rasilimali za chini ya ardhi zitafanywa kwa msingi wa uamuzi wa serikali.

Soma zaidi...

Hizb ut Tahrir / Wilayah Sudan Yakutana na Nazir wa Bani Amer Al-Mutahidah

Ujumbe kutoka Hizb ut Tahrir / Wilayah Sudan ulikutana afisini kwao mjini Port Sudan mnamo siku ya Alhamisi, tarehe 1 Dhul-Qi'dah 1445 H sawia na 9 Mei 2024 M, ukiongozwa na Ustadh Nasser Ridha, Mkuu wa Kamati Kuu ya Mawasiliano ya Hizb ut Tahrir/Wilaya ya Sudan, na wanachama wa Hizb: Abdullah Hussein, Mratibu wa Kamati Kuu ya Mawasiliano

Soma zaidi...

Enyi Waislamu: Mnaona Jinai za Mayahudi kwenye Kivuko cha Rafah, Gaza na kwa hakika Palestina yote. Na Watawala Hawapeleki Jeshi kwa ajili ya Kunusuru; Badala yake Wanapuuza Mistari yao Mekundu! Wameridhika na Upatanishi wa Marekani na Wafuasi wake!

Enyi Waislamu: Inatosha sasa. Ukatili unaofanywa na Mayahudi kwa watu, miti na mawe hauhesabiki! Sasa wanavamia kivuko cha Rafah, ambacho utawala wa Misri ulikichulia kuwa mstari mwekundu ambao haungekaa kimya kuhusu uvamizi dhidi yake.

Soma zaidi...

Tangu tarehe 11 Mei 2012, Naveed Butt, Msemaji wa Hizb ut Tahrir katika Wilaya ya Pakistan Alisalia katika Kupotezwa kwa Kulazimishwa kwa Sababu Anaitetea Khilafah Rashida

Kutekwa nyara kwa Naveed Butt tangu tarehe 11 Mei 2012, ni dhambi kubwa na ukiukaji wa wazi wa haki za binadamu. Hakuna kesi ya ugaidi, uasi au uhaini iliyosajiliwa dhidi ya Naveed Butt. Zaidi ya hayo, hakuna kesi hata ya kumdhuru nzi, au kung'oa jani kutoka kwa mti, ya Naveed Butt mwenye huruma na mkarimu.

Soma zaidi...

Hizb ut Tahrir / Uholanzi: Matembezi ya Amsterdam “Komesheni Mauaji ya Halaiki Mjini Gaza”

Hizb ut Tahrir / Uholanzi iliandaa maandamano katika mji mkuu wa Uholanzi, Amsterdam, kuinusuru Gaza, yenye kauli mbiu “Komesheni Mauaji ya Halaiki Mjini Gaza.” Maandamano hayo yalizunguka mitaa ya Amsterdam, yakisindikizwa na nyimbo za vijana wakitaka kunusuriwa kwa Gaza na kuhamasishwa kwa majeshi ya Waislamu.

Soma zaidi...

Ni kwa kupitia Khilafah kwa njia ya Utume Pekee, na Umoja Halisi wa Ummah, ndipo Makabiliano Madhubuti kwa Jinai Dhahiri za Magharibi na Kutetea Damu ya Waislamu Yatapatikana

Inasikitisha kwamba licha ya nchi za Magharibi kutekeleza jinai za kivita dhidi ya Mujahidina na Waislamu wa Afghanistan katika kipindi cha miaka 20 iliyopita, utawala wa sasa unatafuta maingiliano ya karibu na wahalifu hao, huku ukifanya mikutano ya kisiasa na kiusalama na wanadiplomasia na maafisa wa usalama wa Marekani na Uingereza.

Soma zaidi...

Hizb ut Tahrir / Wilayah Tunisia: Matembezi “Enyi Jeshi la Fahari la Tunisia, Utawala Unawakuwekeni kwenye Mikono ya Adui Yenu na Muuaji wa Watu Wetu huko Gaza!”

Hizb ut Tahrir / Wilayah Tunisia inaendeleza kuinusuru kwake Gaza ambapo mpaka sasa imeandaa matembezi 33 tangu kuzinduliwa cheche ya Kimbunga cha Al-Aqsa, na ina nia ya kuuamsha Umma na majeshi yake hadi wasimamishe dola la Uislamu aliyowafaradhishia juu yao Mwenyezi Mungu.

Soma zaidi...
Jiunge kwa hii RSS feed

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu