Jumapili, 27 Safar 1446 | 2024/09/01
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Huku wakitelekezwa na Serikali Zisizo na Utu za Waislamu, Wanawake na Watoto wa Kiislamu Wakimbizi wa Rohingya Wanakabiliwa na Baa la Njaa, Maradhi na Vifo Nchini Bangladesh

Mnamo Jumapili 17 Septemba, shirika la msaada la ‘Save the Children’ lilionya kuwa wakimbizi wa Rohingya nchini Bangladesh huenda wakafariki kutokana na uhaba wa chakula, makao, na bidhaa msingi za usafi. Zaidi ya Waislamu wa Rohingya 410,000 wamekimbia Myanmar na kwenda Bangladesh tangu Agosti 25 kutokana na kampeni ya mauaji ya halaiki inayotekelezwa na jeshi la Burma. Kwa mujibu wa shirika la UNICEF, asilimia 80% ya wakimbizi hawa ni wanawake na watoto, 92,000 kati yao wako chini ya umri wa miaka 5, na takriban wanawake 52,000 ni waja wazito au wananyonyesha.

Soma zaidi...

Mapinduzi ya Kijeshi Nchini Zimbabwe Ni Mbinu Tu ya Kikoloni ya Kufanyia Ukarabati Nidhamu Mbovu ya Demokrasia Iliyovunda

Mwanzoni ikitambulika kama ghala la chakula la Afrika, mnamo Jumatano iliyopita 15 Novemba 2017; Zimbabwe ilitiwa taharuki ya kisiasa baada ya viongozi wake wa kijeshi kuchukua mamlaka ya nchi hiyo kwa njia ya mapinduzi, wakieneza vifaru ndani ya jiji kuu la Harare na kumueka raisi Robert Mugabe mwenye umri wa miaka 93 chini ya kifungo cha nyumbani.

Soma zaidi...

Chuki za Ofsted dhidi ya Uislamu ni Dhahiri kuwa ni Msukumo wa Uongo

Shule huru ya Kiislamuu inatafuta tathmini ya mahakama kuhusu kushindwa kwake katika kufaulu ukaguzi wa viwango vya ubora wa elimu kwa msingi kwamba katika maktaba yake kuna vipeperushi vyenye zaidi ya miaka 25 vikifafanua juu ya Kongamano la Khilafah lililo andaliwa na Hizb ut Tahrir nchini Uingereza mnamo 1994.

Soma zaidi...

Watoto wa Rohingya Wanadhalilishwa Mikononi mwa Mabudha! Je, Wanaye Mtetezi?

Shirika la misaada la Médecins Frontiéres, limeripoti kuwa zaidi ya nusu ya wasichana katika kambi ya wakimbizi wa Rohingya eneo la Cox's Bazar, Bangladesh ambao limewatibu baada ya kudhulimiwa kimapenzi na kubakwa nchini Myanmar wako chini ya umri wa miaka 18, na wengine wako chini ya miaka 10. Limeeleza kuwa mamia ya wasichana wa Rohingya wamepewa usaidizi wa kimatibabu na wa kisaikolojia katika kliniki yake mjini Kutupalong inayotibu wahanga wa dhulma za kijinsia lakini likasisitiza kuwa hao ni sehemu tu ya wale wanao amanika kudhulumiwa kimapenzi na kubakwa na majeshi katili ya kibudha tangu kutokea kwa kampeni ya mauaji ya halaiki dhidi ya Waislamu wa Rohingya mnamo Agosti

Soma zaidi...

Gharama Kubwa Inayolipwa na Raia Eneo la Deir al-Zour Na Watawala wa Waislamu katika Meza ya Majadiliano kwa Kuketi na Kukutana na Muuwaji

Ndege za kivita za Urusi, kwa mujibu wa vyanzo vya habari vya kimaeneo kutoka Deir al-Zour, zimefanya mashambulizi ya msururu wa mabomu juu ya feri za mtoni zilizokuwa zimebeba maelfu ya raia wanaokimbia eneo la Deir al-Zour kuelekea maeneo mengine, yakisababisha zaidi ya vifo hamsini na maelfu kujeruhiwa, wengi wao wakiwa ni watoto na wanawake.

Soma zaidi...
Jiunge kwa hii RSS feed

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu