Gazeti la Al-Raya: Vichwa Vikuu vya Toleo 299
- Imepeperushwa katika Al-Rayah
- Kuwa wa kwanza kutoa maoni!
- |
Vichwa Vikuu vya Toleo 299
Vichwa Vikuu vya Toleo 299
Mnamo 27 Julai FSB ya Urusi ilitangaza kummaliza yule anayeitwa "gaidi" katika jiji la Khimki karibu na Moscow. Kwa mujibu wa Huduma Maalum, Mtajik Odil Kayumov mwenye umri wa miaka 19 alidaiwa kupanga shambulizi la kigaidi katika sehemu zilizo na umati mkubwa.
Sera ya kuisalimisha Kashmir ilianzishwa na Musharraf kwa maagizo ya Amerika. Sasa, ili kuikomboa Kashmir Pakistan haina chaguo jengine, isipokuwa kutumia nguvu za kijeshi, baada ya serikali ya Modi kufutilia mbali hadhi spesheli ya Kashmir na kuiunganisha kwa lazima na Muungano wa India, ambao huu ni msitari wa mwisho mwekundu kuvukwa na India.
Wilayah ya Syria: Kampeni "HAPANA kwa Uhalifu wa Suluhisho la Kisiasa; NDIO Kuangushwa kwa Serikali na Kusimamishwa Khilafah!"
Shirika la habari la Reuters lilichapisha mnamo 10/06/2020: "…
Milton Friedman, mwanzilishi wa uliberali mpya, aliandika katika kitabu chake juu ya Urasilimali mwaka 1981: Ni mgogoro tu – ima wa kihakika au wa kudhaniwa – huleta mabadiliko ya kweli.
Mnano July 7, 2020 ndani ya Krimea lilipita wimbi jengine la misako na ukamataji ambapo watu 7 waliwekwa kizuizini:
Mandhari ya kisiasa ya Pakistan inazizima kwa minon’gono kuhusu mustakbali wa Waziri Mkuu Imran Khan.
Mawaziri wa fedha na magavana wa Benki kuu wa G-20 wamesitisha uamuzi wa kurefusha mradi wa kuziondolea madeni nchi masikini 73 mbeleni ya mwaka 2020 hadi itakapoamuliwa vinginevyo katika mkutano wao mnamo Oktoba 2020.
Mnamo 2019, Luigi Di Maio, aliyekuwa naibu wa waziri mkuu wa Ufaransa na waziri wa masuala ya kigeni kwa sasa alisema “Ufaransa ni miongoni mwa nchi ambazo zinachapisha fedha kwa nchi 14 za Afrika ikizuilia ukuaji wao wa kiuchumi na kuchangia ukweli kwamba wakimbizi wanatoka na kisha kufa baharini ama kufika katika pwani zetu.”