Gazeti la Al-Raya: Vichwa Vikuu vya Toleo 571
- Imepeperushwa katika Al-Rayah
- Kuwa wa kwanza kutoa maoni!
- |
Wizara ya mambo ya ndani mnamo Ijumaa iliarifu kuhusu marufuku ya Tehreek-i-Labbaik Pakistan (TLP), ikisema kwamba serikali ya kifederali ina “hoja msingi” za kuamini kwamba chama hicho cha siasa za kidini kinahusishwa na ugaidi.
Kwa kuzingatia shambulizi la Marekani dhidi ya Lebanon na kanda hii kupitia uhalalishaji mahusiano na kujisalimisha, na juhudi za Hizb ut Tahrir katika Wilayah ya Lebanon kuzuia shambulizi hili, ujumbe kutoka hizb, ukiwakilishwa na wanachama wa Kamati Kuu ya Mawasiliano na Kamati ya Amali katika Eneo la Kusini, ulimtembelea Mheshimiwa Mbunge Dkt. Osama Saad afisini kwake Sidon mnamo Jumatatu, 27/10/2025.
Kipindi cha “Nampenda Muhammad” kilichozuka kote Uttar Pradesh Septemba hii kimefichua tena utata wa kisaikolojia na kisiasa unaoendesha Chama tawala cha Bharatiya Janata (BJP) cha India. Kile kilichoonekana, juujuu, kuwa mzozo wa sheria na utaratibu kuhusu mabango ya kidini na machapisho ya mitandao ya kijamii, kwa kweli, kinaakisi wasiwasi mkubwa zaidi – udhalilifu unaojificha nyuma ya onyesho la imani ya wengi.
Taarifa ya Chama cha Maimamu nchini Uholanzi (VIN) inadai kwamba ushiriki wa kisiasa ndani ya jamii za Ulaya ni “njia inayoruhusiwa na halali,” na kwamba ushiriki unaweza hata wa kupendekezwa au wa lazima kulingana na hali. Msimamo huu unahitaji kuzingatiwa kwa makini, kwani unaegemezwa juu makisio ambayo hayaakisi vya kutosha uhalisia wa mfumo wa kisekula.
Yale yanayoitwa makubaliano kati ya dola vamizi “Israel” na Hamas, yaliyopangwa na Washington, yanawasilishwa katika vyombo vya habari vya Magharibi na kwa masikitiko pia katika sehemu za ulimwengu wa Kiislamu kama hatua kuelekea amani. Kiulisia, si kitu chengine ila ni marudio ya mtindo wa zamani: mradi wa kikoloni “Israel” unaimarishwa na kulindwa zaidi, huku jinai zake zikifinikwa na vazi la “amani.”
Mnamo 26 Julai 2025, jiji la Kuala Lumpur lilishuhudia maandamano ya ajabu ya umma — maandamano makubwa ya kudai kujiuzulu kwa Waziri Mkuu wa Malaysia, Datuk Seri Anwar Ibrahim. Mkutano huu ulionyesha hasira kubwa na kuchanganyikiwa kwa watu kuelekea uongozi ambao haujashindwa tu kutekeleza ahadi zake za mageuzi, lakini pia umezidisha ugumu wa watu kupitia nyongeza za kodi, ongezeko la ushuru wa umeme, na kupanda kwa bei za bidhaa muhimu.
Hizb ut Tahrir / Malaysia inalaani vikali mwaliko uliotolewa na Waziri Mkuu wa Malaysia, Dato’ Seri Anwar Ibrahim, kwa Rais wa Marekani, Donald Trump — ambaye mikono yake imejaa damu ya Waislamu wa Gaza — kuja nchini Malaysia kuhudhuria Mkutano wa 47 wa ASEAN jijini Kuala Lumpur. Mwaliko huu si tu ishara ya aibu ya kidiplomasia isiyo na msimamo wa kimaadili; ni aibu kubwa kwa hadhi ya Ummah huu, usaliti unaojeruhi dhamiri ya kila Muislamu ambaye bado ana heshima karibu na moyo wake, hasa zaidi watu wa Palestina.
“Jenerali kipenzi cha Trump,” Asim Munir, amejibu kwa udhalimu kampeni yenye nguvu ya Hizb ut Tahrir katika Wilayah Pakistan, ambayo kwayo inataka uhamasishwaji wa haraka wa Vikosi vya Jeshi la Pakistan ili kuikomboa Palestina. Majambazi wa Asim Munir wamewateka nyara matetezi watano, kutoka Lahore, Karachi na Peshawar, na mahali walipo hapajulikani. Udhalimu wa Asim Munir unatarajiwa. Asim Munir hawezi kutenda, sembuse kufikiria, nje ya maagizo ya Trump katika suala lolote, iwe kuhusu Gaza, Kashmir, Afghanistan au rasilimali kubwa za madini za Pakistan.
Vita vya hivi karibuni vya watu wengi kutoka kwa vyama vya kidemokrasia na serikali za mrengo wa kulia vinavyotaka kupigwa marufuku kwa burqa sasa vinajumuisha Australia, Italia na Ureno. Mataifa haya ni sehemu ya kundi kubwa la nchi adui za Ulaya ambazo tayari zimepiga marufuku burqa. Ufaransa, Ubelgiji, Denmark, na Uswizi zinatekeleza marufuku ya kitaifa katika maeneo yote ya umma, huku Uholanzi na Ujerumani, zikiwa na marufuku ya sehemu inayolenga muktadha maalum kama vile shule au afisi za serikali. Nchini Uingereza, mjadala unalenga wafanyikazi, ambapo chama cha mrengo wa kulia cha Mageuzi cha Uingereza kinasema kwamba burqa kama hizo zinazuia uoanishwaji, mawasiliano, na usalama, zikiziita “nembo za mgawanyiko.”