Alhamisi, 19 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/21
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Kwa Kuifuta Katiba ya ‘72 na Msingi wake, Usekula, Watu wameungana katika Kuendesha Nchi Kwa Msingi wa Katiba ya Kiislamu

Enyi Watu, hasa Wanafunzi-Raia Wanamapinduzi! Kataeni jaribio lolote la kuhifadhi mwendelezo wa mfumo wa kibepari wa kisekula uliofeli wa Magharibi kwa kufanya mabadiliko fulani ya kivipodozi kwa jina la marekebisho ya katiba au kuiandika upya. Lazima muimarishe matakwa ya katiba ya Kiislamu na mfumo wa Kiislamu. Unganeni chini ya uongozi wa Hizb ut Tahrir katika kusimamisha Khilafah kwa njia ya Utume, na mutoe wito kwa watu wenye madaraka wahamishie mamlaka kwa Hizb ut Tahrir ili kutimiza matarajio ya watu.

Soma zaidi...

Maldives Yatumbukia Zaidi ndani ya Mgogoro wa Kifedha, huku Ikiyumba Kati ya China na India

Suluhisho la migogoro ya kiuchumi ya Maldives haliko katika kuyumba kati ya dola mbili zinazopiga vita Waislamu na Uislamu. Mfumo wa sasa wa ulimwengu unaleta madhara kwa Waislamu, kiuchumi na kijeshi. Unafanya dola za Waislamu kuwa uwanja wa kunyonywa na wakoloni, na washirika wao, India na umbile ya Kiyahudi. Suluhisho kwa Maldives ni kuwa sehemu ya Khilafah tukufu, kama ilivyokuwa huko nyuma.

Soma zaidi...

Kitengo cha Wanawake cha Hizb ut Tahrir katika Wilayah Tunisia kinazindua kampeni yenye kichwa “Ufisadi wa Elimu Unatokana na Ufisadi wa Serikali, na Marekebisho Yanahitaji Mabadiliko ya Utawala.”

Kwa kuzingatia mgogoro mkubwa unaoathiri sekta zote muhimu nchini kutokana na ushawishi mkubwa wa wakoloni wanaodhibiti taasisi zake kuu, kuzorota kwa sekta ya elimu kumekuwa na athari kubwa sana. Kuzorota huku kunaathiri kila mtu nchini Tunisia— kina baba, kina mama, walimu, na wanafunzi vilevile—kutokana na mshikamano wake tata na pande nyingi zinazopishana.

Soma zaidi...

Ukiritimba wa Kisiasa wa Vifaa vya Ujenzi Zanzibar: Pigo Jengine kwa Masikini

Tunaitahadharisha kwa dhati kabisa serikali ya Zanzibar kuepusha kufadhaisha zaidi sekta ya ujenzi inayofanya maisha ya mtu wa kawaida kuwa magumu zaidi hasa katika harakati zao za kumiliki nyumba. Kwa kufanya na kusababisha hali ya ugumu na ukali katika maisha ya watu ni dhulma za wazi kwa raia na khiyana kwao na itahesabiwa vikali na Mwenyezi Mungu Mtukufu kesho Akhera na kufanya mambo kuwa magumu zaidi katika maisha haya.

Soma zaidi...

Hotuba ya Msemaji Rasmi wa Hizb ut Tahrir katika Wilaya ya Sudan katika Mkutano na Waandishi wa Habari kwa Anwani: Makubaliano ya Entebbe, Bwawa la Al-Nahdha, na Kupuuza kwa Watawala Maslahi Muhimu ya Ummah

Makubaliano ya Entebbe ambayo yanaonyesha wazi njama dhidi ya haki za maji za Misri na Sudan, kiwango cha uzembe wa watawala wa Misri na Sudan, na msimamo wao dhaifu kuelekea njama zinazofanyika.

Soma zaidi...
Jiunge kwa hii RSS feed

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu