Jumanne, 14 Rabi' al-awwal 1446 | 2024/09/17
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Hao ndio Wanajeshi wa Misri, wa Kweli, na hivi ndivyo inavyopaswa kuwa Hasira yao kwa ajili ya Mwenyezi Mungu

Ummah unaendelea kuweka mifano bora kabisa ya kujitolea muhanga, ikithibitisha kwamba ni Ummah ulio hai ambao unaweza kuugua lakini kamwe haufi na hauagi. Kila moto wa hasira unapopungua katika nyoyo za watu wake, wanyoofu huwasha cheche zake na kuwaangazia njia za Mto Nile dhidi ya wale walioasi dhidi ya Ummah wao, wakakiuka matukufu yake, wakanajisi sehemu zake takatifu, na kumwaga damu yake.

Soma zaidi...

Hizb ut Tahrir / Wilayah Tunisia Yawasilisha Barua ya Wazi kwa Waziri wa Sheria

Asubuhi ya Alhamisi, tarehe 01/06/2023, ujumbe kutoka Hizb ut Tahrir/Wilayah Tunisia, akiwemo Mkuu wa Afisi ya Kisiasa Ustadh Abdul Raouf Al-Amiri na Mkuu wa Kamati Kuu ya Mawasiliano Ustadh Yassin bin Yahya, na mjumbe wa Kamati Kuu ya Mawasiliano Ustadh Mwanasheria Fathi Al-Khamiri, na mjumbe wa Afisi ya Habari Ustadh Ahmed Al-Tatar, walimkabidhi Waziri wa Sheria, Bi Leila Jaffal, barua ya wazi kuhusu kukithiri kwa kukamatwa mara kwa mara kwa wanachama wa Hizb ut Tahrir nchini Tunisia.

Soma zaidi...

Uhalifu wa Kivita wa Mkongwe wa Vita Aliyepambwa Zaidi wa Australia ni Akisi ya Sera ya Vita ya Serikali

Madai ya uhalifu wa kivita dhidi ya mkongwe wa vita aliye hai nchini Australia, Ben Roberts-Smith, yalipatikana kuwa "kweli kabisa" na jaji wa Mahakama ya Shirikisho. Jaji huyo alihitimisha kuwa madai ya kuwashambulia na kuwaua Waafghani wasio na hatia na wasio na silaha yalithibitishwa, na kwamba alileta fedheha kwa nchi yake na jeshi la Australia kwa kuvunja 'kanuni za maadili na kisheria' za ushiriki wa kijeshi.

Soma zaidi...

Ujasusi wa Ufaransa Waikanyaga Sheria na Kufichua Ukweli kuhusu Nchi ya Maarifa na Uhuru kwa Kuomba Kufanyika Sensa ya Watoro Shuleni siku ya Idd al-Fitr!!

Gazeti la kila siku la Ufaransa la La Dépêche lilichapisha mnamo Ijumaa, Mei 19, 2023, habari iliyosema kwamba takriban shule mia moja huko Toulouse na vitongoji vyake zilipokea barua pepe kutoka kwa polisi wa Ufaransa wakiomba kiwango cha utoro wa wanafunzi mnamo Aprili 21, 2023, ambayo ilisadifu kuwa ni sikukuu ya Idd al-Fitr.

Soma zaidi...

Bandari Mpya ya Miungano "Uadui kwa Wakimbizi"

Kwa kuwa hapakuwa na mgombea ambaye asilimia ya kura zake zilizidi 50 + 1 katika uchaguzi uliofanyika Jumapili, Mei 14, raundi ya pili ya uchaguzi itafanyika mnamo Jumapili, Mei 28. Kwa sababu ya kauli zilizorushianwa kati ya miungano, vyama na viongozi wakati wa mchakato wa uchaguzi, jamii iligawanywa katika sehemu mbili, na watu wakawa maadui wa kila mmoja.

Soma zaidi...

Uhakiki wa Habari 07/06/2023

Iran ilizindua kombora lake la kwanza la balestiki lililotengenezwa nchini wakati wa hafla moja kwa mujibu wa shirika la habari la serikali IRNA. Kombora hilo lililopewa jina la "Fattah" liliwasilishwa wakati wa hafla iliyohudhuriwa na Rais Ebrahim Raisi na makamanda wa Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC).

Soma zaidi...
Jiunge kwa hii RSS feed

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu