Kupotea Kwa Fedha za “Plea Bargain” Kumefichua kuwa Suala Halisi ni Manufaa ya Kibinafsi na sio Haki
- Imepeperushwa katika Habari na Maoni
- Kuwa wa kwanza kutoa maoni!
- |
Mapema mwezi huu wa Februari 2023, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan alisema kuwa serikali yake inachunguza akaunti ya benki ya nje iliyoko nchini China ambako zimefichwa fedha zilizokusanywa kutokana na ‘Makubaliano ya Kukiri Makosa’ (Plea bargain).