Tukio la Jalalabad: Kuilinda Dawah ni Wajibu kwa Kila Mmoja Wetu
- Imepeperushwa katika Kyrgyzstan
- Kuwa wa kwanza kutoa maoni!
- |
Mnamo tarehe 26 Novemba, Mashababu wa Hizb ut Tahrir waliandaa amali dhidi ya rasimu ya sheria ya “Uhuru wa Dini na Mashirika ya Kidini” katika eneo la Jalalabad. Wiki tatu baadaye, kati ya Disemba 10 na 14, Kamati ya Serikali ya Usalama wa Kitaifa ilifanya msako katika nyumba 21 katika eneo hilo na kuwaweka kizuizini kinyume cha sheria wanachama wa Hizb ut Tahrir. Vikosi vya usalama havikuruhusu wanachama waliozuiliwa (Mashababu) kukutana na mawakili wao na badala yake walifanya uchunguzi mbele ya mawakili waliofunzwa mahususi kwa kesi hii. Kutokana na hali hiyo, Mashababu wetu walizuiliwa kwa muda kwa kipindi cha mwezi mmoja kwa kisingizio cha kusambaza vipeperushi misikitini vinavyopinga sheria hiyo. Kesi ya jinai ilifunguliwa dhidi yao chini ya shtaka la “kuandaa na kuendesha shughuli za itikadi kali.”