Jumapili, 02 Rajab 1447 | 2025/12/21
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Hizb ut Tahrir / Wilayah Bangladesh Yawaalika Watu Wote Watambuzi, wakiwemo Wanasiasa, Wasomi, Waandishi wa Habari na Kizazi cha Vijana cha Nchi Kutazama Kongamano lake la Kisiasa Mtandaoni lenye Kichwa “Bangladesh 2.0: Utegemezi au Ukombozi?”

Hizb ut Tahrir / Wilayah Bangladesh, imeandaa kongamano la kisiasa la mtandaoni lenye kichwa “Bangladesh 2.0: Utegemezi au Ukombozi?” kutoa mwongozo kwa wananchi ili kufikia lengo kuu la Mapinduzi ya Julai 24. Munaalikwa kutazama kongamano hili ili kupata mwamko wa kisiasa na kuamua nini cha kufanya katika hatua hii ya kisiasa nchini.

Soma zaidi...

Umbile la Kiyahudi ndilo Tatizo Kubwa zaidi katika Nchi za Kiislamu Na Waungaji Mkono wake ndio Tatizo Kubwa Zaidi Duniani Ewe Trump!

Vyombo vya habari viliripoti taarifa ya Rais wa Marekani Donald Trump kuhusu Gaza, ambapo alisema, “Gaza ni tatizo kubwa kwa Israel na Mashariki ya Kati.” Hatujamsikia hata mmoja wa watawala wajinga wasio na maana (ruwaibidha) katika nchi za Kiislamu akimjibu, akimwambia kwamba umbile nyakuzi la Kiyahudi ndilo tatizo kubwa katika nchi za Kiislamu, na kwamba nyinyi ndio mnaliruzuku zana za kijeshi na msaada wa kisiasa na kiuchumi. Nyinyi ndio tatizo kubwa katika ulimwengu wote. Mfumo wenu wa kibepari ndiyo sababu ya masaibu ya dunia, na nyinyi ndio sababu ya kugawanyika kwa nchi za Kiislamu katika dola dhaifu na maumbo hafifi tiifu kwenu.

Soma zaidi...

“Kujitawala Wenyewe” kwa Mujibu wa Matakwa ya Wakoloni!

Ardhi zetu za Kiislamu zimekuwa jukwaa la kupigania mali na ushawishi kati ya Marekani na Ulaya. Cha kusikitisha ni kwamba, zana za mapambano haya ni baadhi ya wana wa Ummah, iwe katika serikali au vuguvugu la waasi, kama inavyotokea leo nchini Sudan, wakati wanaoshindwa pekee katika vita hivi ni watu wasio na hatia, wasio na nguvu.

Soma zaidi...

Tanzia ya Mwanachama wa Afisi ya Amiri, Ustadh Ahmad Bakr (Abu Osama)

Amiri wa Hizb ut Tahrir, Wanachama wa Afisi ya Amiri, Diwani ya Al-Madhalim (Malalamiko), na Afisi Kuu ya Habari na Hizb ut Tahrir kwa jumla wanaomboleza kwa Umma wa Kiislamu Mwanachama wa Afisi ya AmIrI, Ustadh Ahmad Bakr (Abu Osama) aliyefariki dunia asubuhi ya leo, 22 Rabi’ Al-Awwal 1447 H sawia na tarehe 14 Septemba 2025 M, akiwa na umri wa miaka themanini na saba.

Soma zaidi...

Mateso ya watu wa Palestina kwenye Daraja la Mfalme Hussein (Allenby) Kati ya Msongamano, Ufisadi, na Mfumo wa Hatari wa Tabaka la VIP

Kwa kuzingatia njama ya dola jirani  za eneo dhidi ya Ardhi Iliyobarikiwa ya Palestina ili kukaza mzingiro dhidi ya watu wake, kuwadhuru, na kuwasukuma kuiacha ardhi yao na kuikabidhi kwa Mayahudi, Daraja la Mfalme Hussein (Allenby au Karameh) linaunda njia kuu ya maisha ya watu wa Palestina kwa ulimwengu wa nje. Hata hivyo, kivuko hiki, ambacho kinapaswa kuwa njia ya usafiri, kimekuwa chanzo cha mateso ya kila siku kwa wasafiri, hasa upande wa Jordan, ambapo mambo ya kibinadamu, ya kiutawala, na ya kisiasa yanaingiliana na kuunda mandhari katili sana.

Soma zaidi...

Enyi Watu wa Jordan na Wanajeshi Wake: Jihadharini na Kundi la Kitengo cha Gilead, Vitisho vya Umbile la Kiyahudi kwa Nchi yenu, na Ushiriki na Utiifu wa Serikali!

Jana, 10 Septemba 2025, kamanda wa Kamandi Kuu ya jeshi la umbile la Kiyahudi alitangaza kuundwa kwa kitengo kipya cha kijeshi, kinachoitwa “Kitengo cha Gilead,” katika Bonde la Jordan, kitakacho kaa kwenye Bonde la Jordan. Kitengo hichi cha kikanda kina jukumu la kulinda mipaka ya mashariki ya Mayahudi katika Bonde la Jordan na Bahari ya Dead. Aliashiria kuwa kuanzishwa kwa kitengo hicho kunajiri ndani ya muundo wa kile alichoelezea kama “masomo ya kujifunza kutokana na kushindwa kugumu kwa Israel mnamo Oktoba 7, 2023.” Uundaji huu mpya unakuja baada ya vitisho vya viongozi wa umbile la Kiyahudi kupanuka hadi nchini Jordan na kwengineko chini ya mwavuli wa mradi wa “Israel Kubwa”, uliotangazwa na Netanyahu, uliobarikiwa na Trump, na kutangazwa wazi na Smotrich, Waziri wa Fedha wa umbile la Kiyahudi.

Soma zaidi...

Ziara ya Ujumbe wa Hizb ut Tahrir katika Wilaya ya Lebanon kwa Mufti wa Sidon na Wilaya zake

Katika muktadha wa mawasiliano na wanasiasa, wanajamii wa Kiislamu huko Sidon, ujumbe kutoka Hizb ut Tahrir Wilayah Lebanon ukiongozwa na Hajj Ali Aslan, Mwanachama wa Kamati Kuu ya Mawasiliano, Mhandisi Bilal Zaidan, Mwanachama wa Kamati ya Shughuli na Hajj Hassan Nahlas, Mkuu wa Kituo cha Sidon, walimtembelea Mheshimiwa Mufti wa Sidon na wilayah zake, Sheikh Salim Sosan.

Soma zaidi...

Hotuba ya Msemaji Rasmi wa Hizb ut Tahrir katika Wilaya ya Sudan - mbele ya Msikiti Mkuu jijini Port Sudan Wito kwa Watu wa Sudan... Msiiruhusu Amerika Kuichana Nchi Yenu na Kuivua Darfur

Enyi Waislamu: Mataifa katika maisha yao yana masuala nyeti, yaani, masuala ambayo mtu anakuwa na msimamo mmoja: yhai chini yao au kifo kwao. Itikadi ya Uislamu imetubainishia sisi Waislamu masuala yetu nyeti; yaani yale ambayo kipimo chake ni uhai au kifo. Miongoni mwa masuala hayo nyeti ni suala la umoja wa dola na umoja wa Ummah. Tulipoondoa suala hili kwenye kituo chake stahiki hapo awali, Amerika, kwa msaada wa baadhi ya watu wetu, iliweza kuichana nchi yetu na kuitenganisha Sudan Kusini, na sasa inaregea kukamilisha kile ilichoanza mwanzo kuchora, kwa mipaka ya damu, dola mpya katika mabaki ya nchi yetu; kwa kuivua Darfur, ambako matukio yanazidi kupamba moto katika kutumikia njama ya Amerika kwa usaidizi wa zana zake ndani na nje.

Soma zaidi...

Kama sehemu ya kampeni iliyoandaliwa na Hizb ut Tahrir/Wilayat Sudan kukwamisha mpango wa kutenganisha Darfur, Hizb ilifanya Visimamo katika miji kadhaa ya Sudan

Kama sehemu ya kampeni iliyoandaliwa na Hizb ut Tahrir/Wilayat Sudan kukwamisha mpango wa Marekani wa kuichana nchi hii kwa kuitenganisha Darfur na Sudan, hizb ilifanya kisimamo katika Msikiti wa Al-Aqit mjini Gadharef mnamo siku ya Alhamisi, Septemba 11, 2025 baada ya swala ya Ijumaa Septemba 12, 2025, miji kadhaa mikubwa ya Sudan ilifanyika visimamo, pamoja na misikiti mikuu ya Sudan yote. Shawak, Singa, Rabak, Madani, Abbasiya, Taqli, Khartoum (Kalakila na Dukhainat), na misikiti miwili mjini Omdurman.

Soma zaidi...
Jiunge kwa hii RSS feed

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu