Gazeti la Al-Raya: Vichwa Vikuu vya Toleo 347
- Imepeperushwa katika Al-Rayah
- Kuwa wa kwanza kutoa maoni!
- |
Vichwa Vikuu vya Toleo 347
Vichwa Vikuu vya Toleo 347
Harakati ya Hizb ut-Tahrir Kenya imezindua rasmi kampeni ya kiuchumi itakayodumu kwa mwezi mmoja. Kampeni hii itaanza tarehe mosi ya mwezi mtukufu wa DhulHijja 1442 Hijria sawasawa na tarehe 11 Julai 2021 na kutamatika Agosti 11.
Kama kawaida, Mahouthi bado wangali wanawazuia Mashababu watatu wa Hizb ut Tahrir - wabebaji ulinganizi wa kusimamisha Khilafah Rashida kwa Njia ya Utume, ambao ni Shaif Al-Shradi, Muhsin Al-Jaadaby na Ayub Al-Shradi,
Mnamo siku ya Jumanne, 07/06/2021, Ethiopia iliiarifu Sudan juu ya kutekeleza ujazo wa pili wa ziwa la Bwawa la An-Nahdha, kwa kiasi cha mita za ujazo bilioni 13.5 za maji, ambayo inasababisha uharibifu wa huduma muhimu za Khartoum na maisha ya wakaazi milioni 20, kwa mujibu wa taarifa rasmi.
Vikosi vya serikali vimeanzisha tena upya umwagaji wao wa mabomu viunga vya Hama na Idlib, Syria.
Mnamo Juni 13, 2021: “Mazungumzo yasio ya moja kwa moja baina ya Tehran na Washington juu ya kufufua mkataba wa nuklia wa Iran wa 2015 yalianza tena mjini Vienna siku ya Jumamosi huku Muungano wa Ulaya ukisema majadiliano hayo yalikuwa “magumu” na Ujerumani ilitaka maendeleo ya haraka…
Mnamo siku ya Alhamisi Julai 1, Waziri Mkuu wa Pakistan Imran Khan aliwathibitishia wanachama wa vyombo vya habari vya China msaada wake kwa sera za serikali ya China huko Turkestan Mashariki.
Mji mkuu wa Sudan, Khartoum, alishuhudia onyesho la mitindo kwa wanawake kwa mara ya pili na mwanamitindo Nermin Qarqafi, lililohudhuriwa na kundi la vyombo vya habari, sanaa na watu maarufu wa jamii.
Wajumbe wa nchi za Troika, na Mwakilishi Maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa nchini Sudan, walimaliza mazungumzo na mkuu wa Chama cha Ukombozi wa Watu-Kaskazini (SPLM-N) Abdelaziz El-Hilu, katika ngome ya uongozi wa harakati hiyo.