Kuangazia Njia ya Shariah Inayofuatwa na Hizb ut Tahrir Kusimamisha Dola
- Imepeperushwa katika Khilafah
- Kuwa wa kwanza kutoa maoni!
- |
Uhalisia wa sasa wa Waislamu leo ni sawa na awamu ya Makka ya ujumbe wa Mtume, kwani wanaishi katika “Dar ul-Kufr” (Nyumba ya Ukafiri) kutokana na kutawaliwa na sheria zisizokuwa zile zilizoteremshwa na Mwenyezi Mungu (swt) na neno “Dar” ni istilahi ya kifiqhi iliyofafanuliwa kwa kina katika vitabu vya fiqh (Fiqh ya Shariah). Hili linalazimu kufuata njia ya mabadiliko ya Makka. Mtume (saw) alifuata hatua tatu kuu katika njia yake ya kusimamisha dola ya Kiislamu.