- |
- Kuwa wa kwanza kutoa maoni!
- ukubwa wa font punguza ukubwa wa font zidisha ukubwa wa font
بسم الله الرحمن الرحيم
Afisi Kuu ya Habari: Angazo Maalum "Baada ya Miaka Ishirini ya Vita vya Msalaba, Afghanistan Yaelekea Wapi?!"
Mnamo 07/10/2001 M, Amerika, kinara wa ukafiri, na mshirika wake Uingereza walianzisha vita vya kinyama dhidi ya Waislamu, waliishambulia kwa mabomu miji ya Afghanistan ya: Kabul, Kandahar, Jalalabad na mengineyo na makombora ya Tomahawk, na kurusha makombora na aina anuwai za silaha. zilitegemea anga, maji na ardhi za Waislamu ambazo ziliruhusiwa kwao na watawala wasaliti, haswa katika Pakistan na Uzbekistan. Hili liliendelea kwa wiki kadhaa mfululizo. Licha ya ujasiri mkubwa na ukakamavu wa hali ya juu ulioonyeshwa na Waislamu katika upinzani kwa wavamizi, kwa silaha hafifu walizokuwa nazo ikilinganishwa na nguvu za wavamizi, walakini ukali wa shambulizi la kikatili kutoka kwa wavamizi na usaliti wa watawala pambizoni mwa Afghanistan ulisababisha kuanguka kwa Afghanistan na kwenda mikononi mwa Amerika mnamo 2001 M.
Idadi ya vifo vya Waafghani katika robo karne iliyopita ilifikia zaidi ya milioni mbili, ikimaanisha kwamba idadi hii kubwa ya wahasiriwa ilishuka tu tangu uvamizi wa Urusi nchini Afghanistan mnamo 1979 M hadi baada ya uvamizi wa Amerika mnamo 2001 M. Kujitolea huku kukubwa kwa Afghanistan kulimalizika, na la kusikitisha sana, ni kuapishwa kwa Hamid Karzai kama mtawala kibaraka wa Amerika nchini Afghanistan.
Hati ya Bonn, ambayo ilianzisha katiba mpya ya Afghanistan mnamo 12/6/2001 M, ilisainiwa na Amerika kutoka Azimio la Baraza la Usalama Nambari 1883 kuiunga mkono, na katiba iliyomo kwenye waraka huo iliipa Amerika dori muhimu katika mavazi ya Umoja wa Mataifa katika kuamua mambo ya ndani na ya nje ya watu wa Afghanistan, na katika kusimamia kila jambo dogo na kubwa nchini Afghanistan, hati hiyo iliainisha uwepo wa Amerika katika kuanzishwa kwa chombo cha kikatiba, katika kuanzishwa kwa shirika la utumishi wa umma, katika kazi na mamlaka ya serikali, na katika mabadiliko yoyote yanayohusiana na sheria za kiutaratibu za taasisi zote za serikali, na katika ufuatiliaji wa tekelezaji wa nyanja zote za makubaliano, ikimaanisha kwamba Amerika imejiweka yenyewe kama mtawala halisi wa dola hii hadi atakapo Mwenyezi Mungu. Na hili ndilo linalodhihirisha siri za Amerika kwamba nia ni kulitawala eneo la Kiislamu, na wala sio kuwepo utawala (huru) kama inavyodai, bali kwamba vita vyake, ambavyo ilivitangaza kwa kisingizio cha kupambana na ugaidi, sio chochote isipokuwa mlango wa vita vya msalaba dhidi ya Uislamu na Waislamu, kukaza udhibiti juu ya nchi yao, na kuutenga Uislamu na maisha yao kama walivyofanya na wanafanya nchini Afghanistan na Iraq, na kama ilivyoandikwa katika mradi wao (Mashariki ya Kati Kuu). Ni vita vya msalaba ambavyo vilivyofichuliwa na amali za jeshi, kisiasa na kielimu zilizofanywa na Amerika ambapo zililipuka katika nchi za Kiislamu. Hakika, Bush Mwana alizifichua tangu siku za mwanzo za matukio ya 9/11, katika hotuba yake tarehe 16/09/2001, ambapo alitangaza kwamba vita vyake dhidi ya ugaidi ni vita vya msalaba, na haikuwa imepita ila siku nne tu tangu mlipuko huo mkubwa, ambazo hazitoshi kukamilisha uchunguzi wa tukio ambapo haiwezi hata kufikia ushuri yake, ambapo inaonyesha kile kilichofichwa katika hazina ya wanasiasa wa Amerika dhidi ya Uislamu na Waislamu. Na ingawa aliviita (vita vya msalaba) kwa kuwakusanya maadui wa Uislamu pambizoni mwake, aliwaleta Waislamu pamoja kumpinga. Na huu ndio upinzani nchini Afghanistan, ulioilazimisha Amerika kurudi nyuma na kutafuta njia mbadala nchini Afghanistan. Katika kipindi cha miaka ishirini iliyopita, vikosi vya Amerika, pamoja na vikosi vya kimataifa (ISAF) na uongozi wa NATO, havikuweza kupanua ushawishi wa uvamizi (kikamilifu) isipokuwa tu katika mji mkuu, huku maeneo yote ya Afghanistan nje ya Kabul yakisalia mandhari ya silaha operesheni za kisilaha ambazo hazikukoma hata siku moja baada ya uvamizi wa Amerika wa Afghanistan.
Hasara ambazo Amerika ilipata wakati wa uvamizi wake wa Afghanistan zinathibitisha kwamba Amerika ilikuwa ikiondoka Afghanistan ikiburuta mkia wa kushindwa bila ya kutoka na mazungumzo ambayo yangeihifadhi kutokana na ushawishi ambao haingeweza kuufikia ndani ya vita!
Na sisi katika Hizb ut Tahrir tunatambua kwamba katika Taliban kuna ndugu ambao ni wakweli wenye ikhlasi basi ni kwa watu hawa ndio tunawaelekea kwa kuwaambia:
1- Sahihisheni jambo hilo na muache kujadiliana na Amerika, ili msiiwezeshe Amerika kufikia lile ambalo haingeweza kulifikia katika vita…
2- Na kinaikeni kuwa kadhia kuu ya Waislamu ni kuregeshwa kwa Khilafah baada ya kutoweka kwa muda mrefu, kwani ni faradhi ya Mwenyezi Mungu (swt) na utiifu kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw)...
3- Na jueni kuwa kushiriki katika utawala wa mchanganyiko wa Uislamu na usekula haukubaliki na Mwenyezi Mungu, kwani Al-Qaqiy Al-Aziz hakubali chochote isipokuwa kizuri ...
Hii ndio haki ﴾فَمَاذَا بَعْدَ الْحَقِّ إِلَّا الضَّلَالُ﴿ "Na kipo kitu gani baada ya haki, isipokuwa upotovu tu?" [Yunus: 32]. Na kufuata haki ndio kutakakoikoa Taliban, nchi hii, na watu wake, na Waislamu wote ... Hivi ndivyo Hizb ut Tahrir anakushaurini, kama tulivyokushaurini mwanzoni mwa utawala wenu kwa kutangaza Khilafah Rashida ya pili kwa njia ya Utume. Mkakataa kisha mkajua kuwa mumekosea kwa kukataa huko kama ilivyo pokewa kutoka kwa Mulla Omar Mwenyezi Mungu amrehemu katika mojawapo ya vikao vyake lakini baada ya kupita zama ... Sisi hapa tena tunaikariri naswaha je, yupo wa kuitikia?
﴾يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا اسْتَجِيبُوا لِلَّهِ وَلِلرَّسُولِ إِذَا دَعَاكُمْ لِمَا يُحْيِيكُمْ وَاعْلَمُوا أَنَّ اللَّهَ يَحُولُ بَيْنَ الْمَرْءِ وَقَلْبِهِ وَأَنَّهُ إِلَيْهِ تُحْشَرُونَ﴿
"Enyi mlio amini! Muitikieni Mwenyezi Mungu na Mtume anapo kuitieni jambo la kukupeni uzima wa milele. Na jueni kuwa Mwenyezi Mungu huingia kati ya mtu na moyo wake, na kwamba hakika kwake Yeye tu mtakusanywa." [Al-Anfal: 24].
Ijumaa, 20 Dhu al-Hijjah 1442 H sawia na 30 Julai 2021 M
- Kufuatilia Angazo kwa Lugha Nyenginezo -
Kalima ya Video ya Mhandisi Salah Eddine Adada (Abu Muhammad)
Mkurugenzi wa Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir
Kuhusu Athari za Vita vya Msalaba nchini Afghanistan
Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Je! Kuna Nini Baada ya Miaka 20 ya Vita dhidi ya (Ugaidi)?
Jumapili, 05 Safar Al Khair 1443 H sawia na 12 Septemba 2021 M
Kwa Maelezo Zaidi Bonyeza Hapa
Al Waqiyah TV: Filamu ya Makala "Mavuno ... Miaka 20 ya Vita dhidi ya Uislamu!"
- Video ya Makala -
Iliyotengenezwa na Chaneli ya Al-Waqiyah kwa ajili ya utolewaji wa vyombo vya habari
Kwa mnasaba wa Kumbukumbu ya Miaka Ishirini ya Vita Amerika na Ulaya dhidi ya Afghanistan na Iraq kwa kisingizio cha matukio ya 9/11 na vita dhidi ya ule wanaouita kwa udanganyifu (Ugaidi).
Jumamosi, 11 Safar 1443 H sawia na 18 Septemba 2021 M
- Tangazo la Video ya Makala -
- Video Kamili ya Makala -
- Al-Waqiyah TV -
[Kipindi cha Maswala ya Umma]
"Kikao Maalum Kuhusu Risala ya Hizb ut Tahrir kwa Viongozi wa Taliban"
"Kikao maalum kuhusu risala iliyotumwa na Hizb ut Tahrir pamoja na ujumbe wa miongoni mwa Mashababu wake bora kwenda kwa uongozi wa harakati ya Taliban mwanzoni mwa Septemba 2021 M.
Wageni wa Kipindi:
Dkt. Muhammad Malkawi / Jordan
Ustadh Muslim Baghlani / Afghanistan
Ustadh Adnan Khan/ Uingereza
Jumamosi, 23 Rabi' al-awwal 1443 H - 30 Oktoba 2021 M
- Sehemu ya Mahojiano ya Kiingereza -
- Sehemu ya Mahojiano ya Kiarabu -
Jibu la Swali Lililotolewa na Hizb ut Tahrir: |
"Athari za Kisiasa nchini Afghanistan" Siku ya Arafah – Jumatatu 09 Dhu al-Hijjah 1442 H sawia na 19 Julai 2021 M |
- Alama Ishara za Angazo -
#أفغانستان | |||
#Afghanistan | |||
#Afganistan |
Matoleo, Majibu na Vijitabu |
"Athari za Kisiasa nchini Afghanistan" Siku ya Arafah – Jumatatu 09 Dhu al-Hijjah 1442 H sawia na 19 Julai 2021 M |
Wilayah Afghanistan |
Amali za Hizb ut Tahrir Kote Ulimwenguni |
Hizb ut Tahrir / Wilayah Afghanistan Amali Zilizo Andaliwa kipindi cha Kampeni ya Kulimwengu, “Ukombozi wa Konstantinopoli Bishara Njema Ikatimia …Inafuatiwa na Bishara Njema Nyingine!” Ijumaa, 15 Jumada al-Awwal 1441 H - 10 Januari 2020 M |
Video |
Wilayah Pakistan: Baada ya Amerika Kushindwa kwa Fedheha nchini Afghanistan, Simamisheni Khilafah Kummaliza Raj Mkoloni wa Kiamerika Jumatano, 11 Dhu al-Hijjah 1442 H - 21 Julai 2021 M
|
Angazo la Vyombo vya Habari
Harakati ya Kiislamu ya Taliban Kuchukua Moja ya Machaguo Mawili |
||
Mbinu ya Amerika na Kupunguza Kisiasa Wanajeshi ndani ya Afghanistan |