Uamuzi juu ya LGBT ni Dhihirisho la Itikadi ya Kisekula na Muundo wa Siasa ya Kidemokrasia
- Imepeperushwa katika Kenya
- Kuwa wa kwanza kutoa maoni!
- |
Mahakama ya upeo nchini Kenya imeamua kuwa jumuiya ya Wasagaji, Mashoga, Wapenda jinsia mbili, Wanaobadili jinsia (LGBTQ) wana haki ya kujumuika. Uamuzi huo sasa unamaanisha hatua ya kukataa kwa Bodi ya Uratibu ya mashirika yasokuwa ya kiserikali (NGOs) kusajili kikundi hiki ni ukiukaji wa haki za binadamu zinazolinda watu wenye msimamo huu wa kingono.