Gazeti la Al-Raya: Vichwa Vikuu vya Toleo 305
- Imepeperushwa katika Al-Rayah
- Kuwa wa kwanza kutoa maoni!
- |
Vichwa Vikuu vya Toleo 305
Vichwa Vikuu vya Toleo 305
Suala la Palestina limewachosha Wamagharibi katika jitihada zao za kuweka ‘suluhisho,’ tokea kuundwa kwa umbile la Kiyahudi katika Ardhi Tukufu ya Palestina. Wamagharibi hawakuweza kupandikiza umbile hili kimaumbile ndani ya umbo safi la Ummah wa Kiislamu, bila kupingwa.
Katika mahojiano ya mnamo 12 Disemba 2012 pamoja na BBC, alipoulizwa kuhusu ni nani atakayeshinda uchaguzi wa Pakistan wa Mei 2013, aliyekuwa Balozi wa Amerika wakati huo Richard Olson alitangaza kwa ujasiri mkubwa, "Farasi wetu ni demokrasia."
Baadhi ya wanafikra katika nchi yetu, Indonesia, wanakataa kuregelea utumiaji wa sarafu za dhahabu na fedha, na kusema kuwa Shari'ah haiagizi kwamba pesa maalum zitumike, wakitumia dalili kwamba Umar ibn al-Khattab alidhamiria kutengeza dirham kutokana na ngozi za ngamia, je rai hii ni sahihi?
Mnamo Jumatano, 16 Septemba 2020, serikali ya PTI iliweza kupitisha miswada minane muhimu, ikiwemo mitatu inayohusiana na Jopo Kazi la wakoloni la Utendakazi wa Kifedha (FATF).
Mmoja wa Mashababu wa Hizb ut Tahrir / Wilayah Sudan katika mji wa El Obeid; ambaye iliubeba ulinganizi huu licha ya ugonjwa wa kisukari, ambao alisababisha kukatwa kwa sehemu ya mguu wake, na pia kusababisha nuru ya macho yake kupungua, na haya yote hayakumvunja moyo kuubeba ulinganizi huu, na kuipenyeza popote alipokuwa.
Jana, Jumanne, 15/09/2020, Amina Aqareb; Msimamizi wa Mambo ya Ubalozi wa Sudan jijini Washington, na Naibu Balozi alishuhudia kutiwa saini kwa Imarati na Bahrain pamoja na umbile la Kiyahudi Mkataba wa Khiyana Kubwa kwa Palestina
Kutokana na hasara kubwa ya mali na kulemazwa kwa usambazaji wa umeme, sehemu kubwa ya Karachi ilisalia imezama ndani ya mchanganyiko wa maji ya mvua na maji taka,
Hizb ut-Tahrir katika Ardhi iliyobarikiwa (Palestina) iliandaa amali katika Msikiti wa Al-Aqsa uliobarikiwa, ambapo ilitoa hotuba kali yenye kushutumu makubaliano ya kusawazisha mahusiano ya Imarati na Bahrain pamoja na umbile vamizi la Kiyahudi
Afisi Kuu ya Habari: Kongamano Kubwa "Kujiweka Mbali na Khiyana Kubwa"